Hali hiyo ilisababisha kusimama kwa shughuli mbalimbali za kijamii
katika Mji wa Mtwara kama vile usafiri wa mabasi, maduka kufungwa na
watu kutotembea Hovyo.
Mtwara. Hofu imetanda baada ya kusambazwa kwa vipeperushi na ujumbe mfupi wa maneno kupitia simu za mikononi ukionya na kuhamasisha wananchi kusitisha kutoa huduma za kijamii.
Mtwara. Hofu imetanda baada ya kusambazwa kwa vipeperushi na ujumbe mfupi wa maneno kupitia simu za mikononi ukionya na kuhamasisha wananchi kusitisha kutoa huduma za kijamii.
Hali hiyo ilisababisha kusimama kwa shughuli
mbalimbali za kijamii katika Mji wa Mtwara kama vile usafiri wa mabasi,
maduka kufungwa na watu kutotembea Hovyo.
Maonyo ya ujumbe huo yaliandamana na msisitizo wa
kusikiliza Bajeti ya Wizara ya Nishati na Madini ili kujua mustakabali
mzima wa gesi na hasa kujua kama upo kinyume na matakwa yao.
Mara kadhaa baadhi ya wakazi wa mkoa huo wamekuwa
wakipinga kitendo cha Serikali cha kusafirisha gesi hadi Dar es Salaama
kwa ajili ya kuzalisha umeme
Wanamtwara hao kwa madai yao wanataka uzalishaji
huo wa umeme ufanyike mkoani humo na msimamo huo umekuwa ukizusha ghasia
na vurugu za maandamano ambapo mali za Serikali pamoja na za watu
binafsi zimekwisha haribiwa.
Wakizungumza mjini hapa, baadhi ya wafanyabiashara
walimlaumu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mtwara kwa kupotosha dhana nzima
ya usambazaji wa vipeperushi hivyo wakidai ni msimamo wa watu wachache.
Walidai kuwa kitendo hicho ni kufikisha kilio chao kwa Serikali na wala hakukuwapo na njama zozote za kufanya fujo.
“Hali iliyopo kwa sasa ni nzuri na wala hatukutaka
kufanya maandamano kwani ndiyo njia pekee tuliyotumia ili kufikisha
ujumbe wetu kwa Serikali,”alisema na kuongeza:
“Tunataka kujua mustakabali mzima unaohusu gesi na
ndiyo maana tulipanga kusitisha huduma ili tusikilize Bajeti ya Nishati
na Madini kwa siku ya leo (jana).”
Hata hivyo,mpango wa wananchi hao ulikuwa kinyume na ratiba ya Bunge kwani liliendelea na mjadala wa Bajeti ta Miundombinu.
Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Maendeleo, Fabiola
Haule alisema kuwa yeye ametimiza wajibu wa kufika shuleni lakini
mahudhurio ya wanafunzi yalikuwa hafifu.
Kutokana na hali hiyo, alisema walishindwa
kuendelea na ratiba ya kawaida ya shule hivyo akaamua wanafunzi wachache
waliofika kurudi makwao.
Source:mwananchi
Source:mwananchi
0 comments:
Post a Comment