Saturday, May 18, 2013

KUWA MAARUFU SI KUANDIKWA VIBAYA

Wasanii
Baadhi ya wasanii hubadilika na kuwa tabia zisizopendeza mara baada ya kuwa na jina hasa katika vyombo vya habari.
 Wasanii wengine huvaa nguo za nusu uchi, kupigana. Takwimu za hivi karibuni zinaonyesha wasanii wengi nchini wanatumia dawa za kulevya na ulevi kupindukia.
Dar. Mwigizaji anayechipukia, Mariam Ismail amesema umaarufu wa msanii hauji kwa kuandikwa vibaya na vyombo vya habari, bali ni kutokana na sifa alizonazo katika kazi yake ya sanaa.
“Umaarufu wa msanii si lazima ajengwe kwa kuandikwa kashfa katika vyombo vya habari bali ni kuitendea haki filamu anayochaguliwa.”
Mariam anaamini anafanya hivyo katika filamu anazocheza kila anapochaguliwa jambo ambalo hivi sasa kila mtayarishaji anahitaji kufanya naye kazi kwa sababu anajua.
Alisema wasanii wengi hasa wa filamu wamekuwa na tabia ya kutengeneza kashfa na wakati mwingine kuvaa nusu uchi ili tu watokeze kwenye vyombo vya habari jambo ambalo linawashushia heshima katika jamii.
“Wasanii tumekuwa na tabia ya kutokujijali, watu wanavaa nusu uchi na malengo yao hasa ni kutokea kwenye vyombo vya habari,” alisema Mariam.

Next Post Previous Post Home

0 comments:

Post a Comment